Letema POS BeiLipia upyaAnza sasa

Mfumo kamili wa biashara yako - tayari ndani ya dakika 5 hadi 10

Mauzo, stoo, madeni, ripoti na zaidi. Jisajili, lipia kwa simu, na POS yako kamili inaandaliwa yenyewe - bila kusubiri mtu, bila kusakinisha chochote.

Anza sasa

Inavyofanya kazi

1
Jisajili
Jina la biashara, simu yako na kifurushi unachotaka.
2
Lipia kwa simu
M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money, HaloPesa au Lipa Namba.
3
Mfumo unaundwa
Database na POS yako vinaandaliwa kiotomatiki, dakika 5 hadi 10.
4
Ingia na uuze
Unapokea anwani na nenosiri kwa ukurasa na SMS.

Unachopata

Mauzo (POS)
Uza haraka, toa risiti, simamia till na zamu.
Bidhaa na stoo
Hesabu za stoo, bei, makundi na tarehe za kuisha.
Madeni na vikumbusho
Wadaiwa wako wanakumbushwa kwa SMS.
Ripoti
Mauzo, faida na mapato kwa kila sekta.
Wafanyakazi
Kila mtu anaona na kufanya kile anachoruhusiwa tu.
Tovuti ya biashara
Ukurasa wa umma wa biashara yako kwa wateja.
Simu na kompyuta
Fungua popote kwenye browser; unaweza kuiweka kama app.
Data yako salama
Kila biashara ina database yake peke yake.

Imeundwa kwa biashara za aina nyingi

Chagua sekta moja au zaidi - menyu na makundi ya bidhaa vinaendana na biashara yako.

Duka la rejarejaDuka la jumlaSupermarketHoteli / LodgeBaa na mgahawaMikate na kekiMavazi na mitumbaBuchaFamasiPembejeo za kilimoVifaa vya ujenziGerejiElektronikiSaluniPhoto studioStationeryMicrofinance

Mipango na bei

Kawaida

  • Mauzo (POS), bidhaa na stoo
  • Risiti, madeni na vikumbusho vya SMS
  • Ripoti za mauzo na faida
  • Sekta zote 17 + tovuti ya umma ya biashara
  • Wafanyakazi wenye ruhusa tofauti
  • Inafanya kazi kwenye simu na kompyuta
Kawaida - Mwezi 1 TZS 30,000
Kawaida - Mwaka 1 Okoa 17%
TZS 25,000 kwa mwezi
TZS 300,000

Anza na Kawaida

Premium

  • Kila kitu cha Kawaida
  • Uhasibu kamili wa hesabu mbili
  • LPO na malipo ya wasambazaji
  • HR na mishahara
  • Matawi mengi na ripoti ya pamoja
  • Fedha za kigeni
  • Nakala za akiba za kiotomatiki
Premium - Mwezi 1 TZS 60,000
Premium - Mwaka 1 Okoa 17%
TZS 50,000 kwa mwezi
TZS 600,000

Anza na Premium

Bei ni za TZS. Kifurushi kikiisha unalipia upya kwa SHOP ID yako; unapewa siku za neema kabla mfumo haujazuiwa.

Maswali ya mara kwa mara

Inachukua muda gani kupata mfumo wangu?

Kwa kawaida dakika 5 hadi 10 baada ya malipo kuthibitishwa. Ukurasa wa agizo unasasishwa wenyewe na utapokea SMS.

Nalipaje?

Kwa simu (STK push) kupitia M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money, HaloPesa au AzamPesa. Pia unaweza kulipa kwa Lipa Namba na kuandika namba ya muamala; tunathibitisha kisha mfumo wako unaundwa.

Nikipata nenosiri wapi?

Kwenye ukurasa wa agizo (mara moja tu) na kwa SMS. Utalibadilisha unapoingia mara ya kwanza.

Kifurushi kikiisha nini kinatokea?

Unapata vikumbusho kabla hakijaisha na siku za neema (3) baada ya hapo. Ukilipia upya mfumo unaendelea mara moja; data yako haifutwi.

Naweza kubadilisha kutoka Kawaida kwenda Premium?

Ndiyo, wasiliana nasi na tutakubadilishia.

Tayari kuanza?

Jisajili sasa na upate POS yako kamili ndani ya dakika 5 hadi 10.

Anza sasa